POLISI WADAI 6 WAMEUAWA SHAMBULIO KENYA, AL-SHABAAB WAKANUSHA
Kundi la wapiganaji la Al Shabaab limesema litatoa taarifa ya uvamizi lililoufanya jana katika hoteli ya kifahari iliyopo jijini Nairobi, nchini Kenya.
Shambulio hilo linakumbusha lile lililotokea mwaka 2013 dhidi ya jengo la maduka ya kifakari la Westgate Mall ambapo wanamgambo hao wa Al Shabab waliua watu wasiopungua 67.
Taarifa toka nchini Kenya zinasema watu sita wamekufa baada ya kundi hilo kushambulia jengo lenye hoteli na ofisi kadhaa nchini Kenya.
Serikali bado haijatoa takwimu kamili za waliopoteza maisha kwenye shambulio hilo.
Siku ya Jumanne (jana) Januari 15 mabomu na risasi zilisikika kwenye jengo moja kubwa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Polisi na mashahidi wamezungumzia shambulio hilo na kusema kuwa ni la kigaidi. Ndani ya jengo hilo kuna hoteli kubwa inayojulikana kama Dusit D2, benki na ofisi.
Kwenye mlipuko huo magari kadhaa yalishika moto na watu walilazimika kukimbia na wengine kuhamishwa toka eneo hilo. Risasi ziliendelea kufyatuliwa kwa dakika kadhaa ambapo moshi mkubwa ulitanda katika eneo hilo.
Msemaji wa polisi, Charles Owino, amesema maofisa zaidi wa polisi ikiwa ni pamoja na vikosi vya kupambana na ugaidi walipelekwa katika eneo la tukio.
Magari ya kusafirisha wagonjwa, na askari wa zimamoto walipelekwa pia katika eneo hilo.
Wanamgambo wa itikadi kali wa Al Shabab wamedai kuhusika na shambulio hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment