KIKOSI cha Simba kimegeuza Uwanja wa Taifa kuwa machinjio yao kimataifa na kuanza kujibebea pointi zao tatu kibabe kwa wapinzani wa kimataifa.
Simba ambao kwa sasa wanaipeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa wanaongoza kundi D, ambalo lina timu kama Al Alhy ya Misri, JS Saoura ya Algeria na AS Vita ya Congo.
Mchezo wa kwanza wa kimataifa Simba Uwanja wa Taifa ulikuwa ule wa hatua ya awali dhidi ya Mbabane Swallows walishinda kwa mabao 4-1 na mchezo wao wa pili ni ule uliowapa tiketi ya kushiriki hatua ya makundi ulikuwa dhidi ya Nkana FC ambao waliwachinja kwa mabao 3-1 .
Mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi walianza na JS Saoura ya Algeria ambao nao katika Uwanja wa Taifa walichinjwa kwa mabao 3-0.
Katika michezo mitatu waliyocheza Uwanja wa Taifa ya kimataifa Simba wamefanikiwa kufunga jumla ya mabao 10, huku wakiwa wamefungwa jumla ya mabao 2 na kufanikiwa kupata Cleanshit moja na pointi tatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment