BAADA YA KUMVUA UNAHODHA YONDANI, JUMA ABDUL ATOA TAMKO KUHUSIANA NA ZAHERA
Baada ya Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kumvua kitambaa cha unahodha, Kelvin Yondani na kumpa kitambaa Ibrahim Ajibu, Juma Abdul amesema wala hana noma nae.
Ajibu amepewa majukumu mapya na kocha huyo kwa kile alichoeleza kwamba amebadilika tofauti na mwanzo hivyo anaamini atafanya mambo makubwa.
Abdul ambaye alikuwa msaidizi wa Yondani na sasa anaendelea kufanya kazi hiyo kwa nahodha mpya, alisema anaheshimu maamuzi ya mwalimu na atafanya kazi kwa ushirikiano na bosi wake mpya.
“Hakuna tatizo lolote kwangu nitafanya kazi na Ajibu hasa baada ya kushirikiana na Yondani, kuna mengi tumefanya naye kwa kushirikiana na matokeo yameonekana natumaini itakuwa hivyo kwa Ajibu,” alisema Abdul ambaye amepoteza namba yake kwenye kikosi cha kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment