January 6, 2019


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems ameamua kupanga kikosi Full Masinondo katika mechi ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM, ikielezwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya JS Saoura ya Algeria.

Mashabiki wengi walishangazwa baada ya kikosi cha Simba kuonekana kikiwa sawa na kile ambacho Simba hukitumia kwenye Ligi Kuu Bara.

Sehemu ya benchi la ufundi la Simba limeeleza: “Kocha ameamua kufanya match fitness. Kutaka wachezaji wawe fiti zaidi. Baada ya mechi hiyo wataendelea na mazoezi.

“Lengo ni kujiandaa na Waalgeria halafu pia kuwafurahisha kwa kuwa KMKM ni timu inayoheshimika Zanzibar na mashabiki Simba pia wanataka furaha. Itakuwa mechi ya ushindani na hakuna utani,” kilieleza chanzo.

5 COMMENTS:

  1. Match Fitness Na Kutufurahisha Tuna Hitaji Magoli Mengi Sisi Pia Watu Kama Zana Watumie Nafasi Vizuri Ana Mwili Mkubwa Kinacho Mponza Pupa Atulie Atuoneshe Kile Tunacho Taka Wadau Wa Soka Maana Tuliambiwa Ni Mrithi Wa Kapombe Lakini Ajabu Ni Kwamba Gyan Ana Mweka Benchi

    ReplyDelete
  2. Hata Gayani alitarajiwa kuja kuwa mrithi wa mavugo akaishia kukaa benchi na kama Viongozi wa Simba wangekuwa wanasikiliza kelele za Mashabiki ambao wengi wao hawana uweledi wowote kuhusu makuzi ya mchezaji basi hii leo tunavyozungumza Nicholasi Gayani keshatimuliwa zamani sana pale Simba .Leo hii hapana shaka Gayani ni miongoni mwa wachezaji lulu pale Simba na mwenye kila dalili yakuwa miongoni mwa wachezaji wa kutumainiwa kikosini. Ukiifuatlia historia ya Thienry Henry na Arsenals utagundua yakuwa alisota pale kiasi cha mashabiki wasiokuwa na weledi au subra kuanza kumponda na kumkejeli kuwa ni mchezaji wa hovyo lakini mwisho wa siku Thiery Henry alikuja kuondoka Arsenals kwa heshima. Zana coulibaly hata miezi miwili hajatimiza pale simba lakini tayari mashabiki maandazi washaanza kelele za mchezaji gani, jamani?

    ReplyDelete
  3. Yesi kuwapumzisha wachezaji wakati game keshokutwa sio poa so kocha yuko sahihi

    ReplyDelete
  4. Kwa taarifa za uhakika tunaambiwa Makachero wa As Vita tayari wapo Zanzibar kuichimba Simba.Utaona kwa jinsi gani wenzetu walivyomakini katika kutengeneza mazingira ya Ushindi kabla hata mechi haijaanza. Inawezekana kabisa wana watu tayari nchini Algeria na Misri kufuatilia wapinzani wake wengine pamoja na kuweka mazingira rafiki ya timu yao itakapokwenda huko. Cha kujiuliza je Simba tayari ilishapeleka watu wao wa kazi kwa wapinzani wake kupata taarifa muhimu au wanasubiri majaaliwa ya Mungu? Ninachokijua mimi majaaliwa ya Mungu yanasubiriwa baada ya mtu kuyafanyia kazi na sio kubweteka na kusubiri. Hawa watu wa As Vita ya Congo waliopo Zanzibar hakika hawataondoka hapa nchini mpaka mwchi zao mbili na Simba zikamilike za Nyumbni na ugenini. Kwa maana hiyo watu hao wa As Vita wataishuhudia mechi ya Simba ikicheza na Js Soura ya Algeria ili kukamilisha mkanda mzima wa taarifa za Simba kabla ya kucheza na As Vita. Tunaimani viongozi husika wataendana na kuzikabili fitna hizi kikamilifu bila kuchelewa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kachero mkuu na mwenyeji wa As Vita, JS Soura na wamisri ni Shaffii.. Ndo wahuni wanavoishi mjini!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic