Siku moja baada ya kuuzwa Misri, kiungo Shiza Kichuya ametolewa kwa mkopo.
Kichuya ameuzwa na Simba katika klabu ya Pharco ya Misri ambayo imeamua kumtoa kwa mkopo Enppi inayoshiriki Ligi Kuu Misri.
Kiungo huyo tayari ni mali ya Mafarao hao na atamalizana na Simba wikiendi hii katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba iko nchini Misri kuwavaa wababe wa Afrika, Al Ahly
Naona kizungumkuti au kwa kuwa ni maamuma wa biashara za wachezaji, kwa nini simba isimuuze moja kwa moja kwa timu anayotolewa mkopo ama badu huu ndio ule msemi usile na kipofu ukamshika mkono
ReplyDeletekaza babu ukaiwakilishe simba kimataifa na tz kiujumla
ReplyDeleteMbona dau hamtaji au kauzwa bure
ReplyDeleteIssue kubwa hapa ni kuwa Simba wamechezewa kiini macho kupoteza mchezo wao. Kwa nini wasisubiri kumaliza mauzo ya mchezaji baada ya mechi yao? Hii itapelekea wachezaji kupotea kisaikolojia wasiwekeze kwenye kuchukua pointi...
ReplyDeleteDidisha la usajili misri limefungwa Jana sasa itawekana vp kusubiri mechi
Delete