January 13, 2019


MCHEZO wa Simba Queens na Yanga Princess ambao unatarajiwa kucheza leo, timu zote mbili zimepania kupata ushindi kwenye mchezo huo wa Ligi ya Wanawake maarufu kama Serengeti Women's Premier League utakaochezwa Uwanja wa Karume.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana kwenye Ligi ya wanawake kwa kuwa Yanga Princes wamepanda Ligi msimu huu na Simba walikuwepo msimu uliopita.

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Omary Mbezwe amesema maandalizi yao yapo tofauti na maandalizi ya michezo mingine kutokana na ugumu uliopo.

"Nimepata bahati ya kuwatazama na kuwafuatilia, wana timu nzuri na wachezaji wenye morali, hivyo nimewaambia wachezaji wangu wanapaswa watafute matokeo mapema ili kuweka historia kwa kuwa ni mara yetu ya kwanza kukutana," alisema Mbweze.

Kocha wa Yanga Princess, Hamida Kinonda amesema wanatambua wapinzani wao ni makini, wanakazi ya kupata matokeo ndani ya dakika tisini jambo ambalo linawezekana.

"Kila timu inahitaji ushindi, tunaingia Uwanjani hesabu kubwa ikiwa ni kupata matokeo, wachezaji wanajua ushindani uliopo, naamini watacheza kwa umakini na kufuata maelekezo," alisema Kinonda.

Simba Queens imecheza michezo minne ikiwa nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia pointi 10, Yanga Princess wapo nafasi ya saba baada ya kucheza michezo minne wakiwa na pointi sita.

2 COMMENTS:

  1. Saleh jembe hawawezi weka matokeo endapo timu wanayoifagilia imepigwa zaidi ya mkono kwa bila

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic