January 11, 2019


ZIKIWA zimebaki siku mbili ili uchaguzi wa Yanga ufanyike uongozi wa Yanga umetaja sifa za viongozi ambao wanapaswa wapewe nafasi ya kuongoza timu yao.

Wanachama wa Yanga wanatarajiwa kufanya uchaguzi Januari 13, uchaguzi utakaofanyika katika ukumbi wa Polisi Messi Oystebay kuanzia saa moja kamili asubuhi na wanachama wenye kadi za benki pamoja na zile za kitabu ndio wanaruhisiwa kuchagua viongozi.

Mjumbe wa kamati ya Utendaji na Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Siza Lyimo amesema kuwa kiongozi bora ni yule anayefuata misingi bora ya uongozi ikiwa ni pamoja na uadilifu.

"Kiongozi bora anajengwa na misingi ya uadilifu, hivyo huwezi kuongoza kama hauna hulka ya ujasiri na kuwa muungwana katika mambo ambayo unayafikiria ama kuyatenda.

"Wale ambao wana hulka za kuwadanganya wapiga kura kwa kutoa rushwa ili wachaguliwe wanajivua sifa za kuwa viongozi, ni wajibu wa wanachama kuchuja na kujua aina bora ambao tunahitaji waweze kutupa kile ambacho tunahitaji," alisema Siza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic