NA SALEH ALLY
NINGEKUWA ni kiongozi wa Yanga au Simba, kitu cha kwanza kabisa ambacho ningefanya ni kuwaomba radhi wadhamini wakuu wa klabu ninayoiongoza.
Wadhamini wakuu wa Yanga na Simba ni SportPesa, kampuni kubwa zaidi ya michezo ya ubashiri hapa nchini.
Kampuni hii kila mwaka inamwaga zaidi ya Sh bilioni moja kwa Yanga na nyingine kama hizo kwa Simba. Katika historia ya klabu hizo, huu ndio udhamini mkubwa zaidi kuwahi kutokea.
Nasema ningewaomba radhi kutokana na mambo ambayo yamekuwa yakijitokeza na kuwakatisha tamaa katika hali ya kupindukia kupita kiasi.
SportPesa wamekatishwa tamaa hadi inatia huruma kwa kuwa timu wanazozidhamini kutoka Tanzania zimekuwa kichekesho kila inapofanyika bila kuangalia ni Kenya au Tanzania.
Kila mara ni timu nane, nusu kutoka Tanzania na zilizobaki Kenya. Mara zote tatu wanachukua Wakenya, jambo ambalo linaonyesha hakuna majuto kwa timu za Tanzania kuanzia kwa viongozi na wachezaji wenyewe.
Wachezaji wanaochezea timu za Tanzania si wapambanaji, hawajutii wala si wanaotaka kuona hawashindwi. Ndio maana unaona fainali ya kwanza vigogo wa Kenya Gor Mahia na FC Leopards, waliingia kwenye ardhi ya Tanzania.
Fainali ya pili, Simba wakajitutumua wakiwa ugenini wakaingia fainali na kupigwa. Mara ya tatu, hakuna Simba wala Yanga na hii ni Tanzania tena.
Aibu hii, kwa wale wanaojitambua lingekuwa jambo baya sana. Lakini linaweza kuonekana ni la kupita kwa kuwa wahusika wanachukulia poa.
Huenda ukiwa mchezaji, kama unaona hauna akili za kujituma, basi jifunze mambo. Huenda kama wachezaji wangejua SportPesa wangetamani angalau kuona timu ya Tanzania nayo inafuzu.
Hii ni kuondoa upepo kama mashindano ya Kenya, kuachana na kuwa na ladha inayofanana lakini pia, hata zawadi zinapokwenda nchi tofauti na timu kama Everton inapotua kucheza nchini pia ni faida.
Yanga na Simba ni watu kutoka nchi gani, wasiowaza wala kujua kwamba SportPesa kweli ni wadhamini lakini ni wafanyabishara pia.
Hivyo wanachokitoa, kawaida wangependa wafaidike kwa maana ya biashara yao. Hivyo timu za Tanzania kufanya vema kwa kuwa mdhamini wao ni SportPesa Tanzania!
Viongozi nanyi mnakuwaje na wachezaji wanaoshindwa kila siku. Wachezaji wasiobadilika au kujitambua na kuelewa maana ya faida.
Aibu ya namna hii mtaipata hadi lini na kama ni suala la wadhamini wenu, nao watafurahi lini. Maana timu kama Everton ikija kucheza hapa kama ilivyokuwa ni faida kubwa.
Wadhamini wenu wanatoa fedha nyingi sana, lengo lao ni biashara kweli lakini mnafaidika sana na ndio maana wachezaji kama Simba na Yanga mnalipwa mishahara mikubwa hata kama inachelewa.
Vipi hamtambui umuhimu wa SportPesa. Mfano kama sasa hivi, timu zilizoingia fainali au bingwa na mshindi wa pili hakuna anayedhaminiwa na SportPesa.
Zilikuwa timu nne ambazo mbili za Tanzania, Simba na Yanga, usishangae siwataji Singida United kwa kuwa walishamaliza mkataba. Halafu Kenya Gor Mahia na AFC Leopards ambazo hakuna iliyokwenda fainali.
Maana yake kwamba hata hao SportPesa wanaweza kuwa wanaona waliowadhamini si watu makini hata kama wana mtaji wa watu. Hii si sawa na si jambo sahihi kwa anayetoa fedha yake naye akitegemea kupata faida.
Kuna kila sababu ya viongozi nanyi kubadilika, wachezaji wanaoshindwa kuonyesha faida, achaneni nao hata kama mashabiki watanuna.
Simba nimeona mashabiki wakiwashambulia viongozi pamoja na kwamba walioboronga ni wachezaji lakini mnapozidi kuwaachia kwa kisingizio eti mashabiki wataona mnawaonea, basi wataendelea kuwaharibia na kuna siku mtakosa kabisa wadhamini ili nao wacheleweshewe mishahara na ndio watajua umuhimu wa wadhamini.
Hivi mwandishi haya mashindano lazima ubingwa wachukue Simba au Yanga ndio yaonekane yamefanikiwa.
ReplyDeleteEnter your comment...kaka umefeli
ReplyDeletekama wanataka hela si wangewapanga simba na yanga kundi moja .....kwahyo hauziheshimu team za kenya mfano gor mahia ambae kaingia tena makund mwaka huu shirikisho
ReplyDelete