January 28, 2019


MLINDA mlango wa Mbao FC, Metacha Mnata ameibuka shujaa wa Tanzania baada ya kuwa mlinda mlango bora wa michuano ya SportPesa Cup iliyomalizika jana Uwanja wa Taifa na kikosi cha KK Sharks kuibuka mabingwa nafasi ya pili ikibebwa na Bandari zote za Kenya huku Tanzania Simba ikiambulia nafasi ya tatu.

Katika tuzo za jumla ni mchezaji mmoja tu kutoka Tanzania ambaye alibeba tuzo ambaye ni Mnata alibeba tuzo ya jumla ya golikipa bora pia katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu aliibuka mchezaji bora wa mechi.

Kutokana na kuwa mchezaji bora wa mechi Mnata alipewa zawadi ya dola 500 na tuzo ya golikipa bora wa mashindano ya SportPesa Cup.

Tuzo nyingine za jumla kama mchezaji bora wa mashindano ilibebwa na William Wadri wa Bandari na ile ya mfungaji bora ambayo msimu uliopita ilikuwa kwa Meddie Kagere ikibebwa na Abuye Duke wa KK Sharks.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic