January 11, 2019







Mtanzania Thomas Ulimwengu, ametua nchini na kikosi cha JS Saoura cha Algeria tayari kuwavaa Simba.

Kikosi hicho kutoka Algeria, kina kibarua dhidi ya mabingwa hao wa Tanzania katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi na mechi itapigwa kesho.

Ulimwengu mwenye uzoefu na michuano hiyo ameonyesha kuwa mtulivu na mwenye tabasamu bashasha.

Akizungumza mara baada ya kutua uwanjani hapo Ulimwengu alisema: "Nina furaha kurudi kucheza tena nyumbani, Simba ni timu nzuri lakini sisi tumejiandaa kwa ajili ya kupambana nao."

JS Saoura watacheza na Simba katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

5 COMMENTS:

  1. Safi sana Thomas unajielewa umetuia maneno machache yenye busara kwa sababu upo kazini Algeria lkn bado Tanzania ni kwenu so pote panastahili heshima. Umeonyesha utofauti mkubwa na yule dogo asiye na heshima Kessy kwa jinsi alivyokuwa akiwazihaki simba muda wote. Mimi sikuwa kumuona chama akiwazihaki Nkana hata pale alipofunga goli la ushindi alishangilia kisha akarudi uwanjani lkn ingekuwa kessy amefunga cha kwanza najua angekimbilia kwenda kuwatusi upande wa mashabiki wa simba kwa sababu hana adabu wala fadhila

    ReplyDelete
  2. Kessy professional football haiwezi alienda kule bahati mbaya

    ReplyDelete
  3. Jaman Mmesahau Kumtaja Abdi Banda Naye Yupo Kama Kessy Tu Ulimbukeni Wake, Nawatakia Ushindi Mzuri Watani Zangu Simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic