January 28, 2019

Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumpa faraja mzazi ni pamoja na kumuona mwanae anapiga hatua za kimaendeleo kila siku, na ndicho haswa kilichomgusa na kumfurahisha Mama Mzazi wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, katika usiku wa mwanae huyo alipokuwa akizindua pafyumu yake sambamba na taasisi yake ya kushugulikia na kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi inayoitwa 'Haji Manara Foundation'.

Hafla ya uzindui huo imefanyika usiku wa Januari 27, katika ukumbi wa Hyatt Regency na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali akiwemo Naibu Waziri wa Vijana, Antony Mavunde, Mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda, pamoja na mastaa kutoka katika tasnia mbalimbali nchini akiwemo mwanamuziki Diamond Platnumz.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic