MKURUGENZI wa Ufundi wa Gwambina ambaye alikuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya DR Congo, Mwinyi Zahera, ametolea ufafanuzi suala la kuachwa kwa nyota wawili wa Yanga, Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe kwa kusema hawawezi kupata nafasi kwenye timu hiyo ya taifa.
Tuisila na
Tonombe walijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha kubwa mwaka huu wakitokea
AS Vita ya DR Congo.
Zahera
amesema kuwa nyota hao wa zamani wa AS Vita hawawezi
kupata nafasi kwenye kikosi hicho kutokana na ushindani wa namba uliopo.
“Nimeona
kikosi cha Timu ya Taifa ya Congo kilichoitwa hivi karibuni ili kujiandaa na
michezo miwili dhidi ya Burkina Faso, Oktoba 9 na baadaye dhidi ya Morocco na
najua watu wengi hasa mashabiki wa klabu ya Yanga wamekuwa wakijiuliza kwa nini
nyota wao, Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe hawajaitwa.
“Hapa jibu
ni rahisi tu, timu ya Taifa ya Congo ina wachezaji zaidi ya 400 ambao wanacheza
barani Ulaya, yupo mchezaji anayecheza Ligi Kuu nchini Ufaransa ambaye anacheza
nafasi moja na Kisinda naye hajaitwa kwenye timu kwa sababu wapo wachezaji
wanaocheza kwenye nafasi zao walio kwenye ligi bora zaidi, hawa ndiyo wanapewa
kipaumbele wakati wa kuita timu ya taifa.
“Ndiyo maana
licha ya kwamba Tonombe na Kisinda wote wametoka As Vita ambayo ilikuwa
inafundishwa na kocha wa timu ya Taifa ya Congo, lakini hawakuwahi kuitwa
kwenye kikosi cha timu ya taifa,” amesema Zahera.
Utetezi wa kitoto sana. Sema tuu hawana uwezo huo.
ReplyDeleteTrue! kweli wasipepese macho Wala wasitikise masikio, waeleze ukweli tu hawana uwezo hao wachezaji
DeleteKwa maelezo ya kocha msaidiz wa timu ya taifa ya Congo MWINYI ZAHERA,Kumbe TONOMBE NA KISINDA hawajawahi kuitwa timu ya Taifa ha ha ha ha ha ha CHIRWA ameitwa.itabidi waitwe TAIFA STARS maana sifa tunazopewa kwamba wapo first eleven ya taifa sasa iweje??
ReplyDeleteKwa hiyo Eng. Hersi alitudanganya kwamba ni wachezaji wa timu ya taifa ya DRC?
ReplyDeleteNaona wanangu wa msimbazi mnateseka Kwan mugalu ameitwa?
ReplyDeleteMajibu ya swali hilo kamuulize MWINYI ZAHERA au mjomba enu,ukweli utabaki palepale kwamba hawana uwezo wa kucheza timu ya Taifa,na hata aliposajiliwa CHIRWA pia tuliambiwa anachezea timu yake ya Taifa ila juzi kwa kinywa chake anasema ndio mara yake ya kwanza kuitwa kwenye timu ya Taifa na anaona fahari kuu,bado yaliyojificha yatajulikana muda sio mrefu japo tayari tunafahamu fika kwamba wapo hapo kwa mkopo
DeleteDah! kula tano 👊 bonge la point, hili yawezekana likawa Kama la makambo.
DeleteKwahyo kwaakili yko ulitaka iweje wawe kwamkopo wasicheze timu ya taifa we inakukera nini tunacho jua ni wachezaji wa yanga au ulitaka waitwe ili ufaidike nini ndo maana mnapigwa kumbe wambea hvo
DeleteMmmmhhh hilo nalo neno
ReplyDeleteHalafu Timu ya Taifa ya Congo DRC ni tofauti Sana na Zambia, Tanzania,Rwanda ,na sijui Kenya msilete Uswahili ndiyo maana Mugalu Chris Kaitwa ,Mikia hoyeeeee
ReplyDeleteWapo kwa mkopo nao mnawavizia?Mwandae Hans Pope Tena Kamati ya maadili
ReplyDeleteTatizo mikia mmesajili wachezaji ambao kwenye timu za taifa wanaocheza nje walio wengi ni Tanzania sasa kwann wasiitwe. Umeambiwa kuna mafundi wengi wapo ulaya kwenye ligi bora sasa hapo lipi hamjaelewa. Lakin wangekuwa wanatoka kwenye nchi ambazo ninyi mnasajili wangekuwa first eleven.
ReplyDeleteZambia toka China anunue nchi mpira bye-bye eti Timu ya Taifa Zambia inategemea Chama wa Simba au Larry Bwalya ,hao na Zanzibar hapana tofauti.
ReplyDeleteTimu ya Congo ina mapro wengi wanakipiga ulaya, hii ligi yetu haiwezi kushindana na ligu za majuu, hao zambia wanawachezaji gani wanacheza ligi bora ulaya?
ReplyDeleteHakuna ndio maana unaona skina Chama wanaitwa.
Hamna kitu hpo uwezo msg
ReplyDeleteNyie mliambiwa mapema kabisa wale wanacheza timu ya taifa ya wachezaji wa ndani, yaani CHAN, Sasa mlitaka nini tena kama hamukuelewa mwanzo si mngeuliza?
ReplyDeleteManyani mabishi kweli yanapoint za kijinga ili mradi yaonekane na yao yameongea
ReplyDeleteChaka hilo.
DeleteBasi Mugalu Kaitwa,ila mkubali Zambia kwishneeee.Huyo Bwalya Larry na Ndemla hapana tofauti
ReplyDeleteHapa kwetu Ndemla National Team hata hafikiriwi Sasa Zambia si ndo bye-bye?