UONGOZI wa Simba umesema kuwa sababu kubwa ya wao leo kuifuata JKT Tanzania, Dodoma kwa basi ni kutimza ombi la mashabiki wao wa Morogoro ambao waliwaomba wawapelekee taji la Ligi Kuu Bara ambalo walilitwaa msimu wa 2019/20.
Simba leo inaanza safari kuifuata JKT Tanzania, Dodoma kwa ajili ya mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 4, Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanatimiza maombi ya mashabiki wao wa Morogoro ambao wameomba wapelekewe taji la ligi.
"Kikosi kitaondoka kwa basi kuelekea Dodoma na sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kutimiza ombi la mashabiki wa Morogoro ambao waliomba tuwapelekee taji letu la ligi ambalo tulitwaa msimu uliopita.
"Hivyo kwa kukubali ombi letu la mashabiki wa Morogoro tutakuwa na kombe letu, mashabiki watapata muda wa kuliona kombe letu na Jumamosi tutaanza safari kuelekea Dodoma ambapo tutapata muda wakufanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuikabili JKT Tanzania," amesema.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteNakweli ukiangalia Yanga wana ela kweli si ndo mana wakawachukua kwa mkopo Tusila Kisinda na Mukoko, ata Carlinhos ni mchezaji wa gharama kweli, yule Michael Sarpong (Yipke aliyechangamka) ata Tp Mazembe walikuwa wanamtaka ila Yanga wamemchukua ! utopolo ela ela wanayo
ReplyDeleteSafi kabisa
DeleteApo saw mmewatendea haki mashabik wetu
ReplyDeleteHata hivyo, Dodoma si mbali kivile hadi timu igharamie usafiri wa ndege. NI sawa tu na mashabiki huko njiani, hasa Morogoro, wawaone na wapige picha na kombe lao.
ReplyDeleteHao kandambili inawauma roho
ReplyDeleteMbona kombe hamkwenda nalo kipindi mnadroo , acheni uhuni nyie MISUKULE fc na huyo mzungu pori wenu anawapotosha tu na nyie kwakuwa ni manyumbu mnakubali
ReplyDeleteKwenda nalo si mpaka uombwe? Au unadhani km saa vile popote unaivaa tu
DeleteKwenda nalo si mpaka uombwe? Au unadhani km saa vile popote unaivaa tu
DeleteKiukweli Simba ni Timu ya WATU, hivyo unapo pata taarifa kwamba wanataka KOMBE LAO, ukiwa na akili timamu lazima utatekeleza kwa upendo na hekima.Tunapongeza maamuzi mliochukuwa, tunashauri mjitahidi kufika Dodoma mapema wachezaji wetu wa punzike kwa ajili ya mchezo wetu na JKT Tanzania. Nitakuwepo Uwanjani kushudia hili nikitokea Korogwe - TANGA, Tanzania.
ReplyDeleteMambo ya simba sijui yanga yanawauma Nini kweli manara aliposema atahakikisha kila mtanzania anaishabikia Simba hakukosea
ReplyDeleteMwanangu waga nakuona wamaana sana kumbe bonge la boya hvi kwa akili yako yote hyo unafata ujinga wa manara yule chizi ni sawa na wanao sema kibaki chama kimoja jua kichan matope
Delete