September 24, 2020


OFISA Habari wa Simba, Haji Manara, amewaomba mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi kuhusu tetesi za mchezaji wao, raia wa Zambia, Clatous Chama, ambaye anadaiwa kuwa mkataba wake uko karibuni kumalizika hivyo ataondoka klabuni hapo huku akihusishwa kujiunga na Klabu ya Yanga SC.

 

Manara amesema hayo leo leo Septemba 24, alipotembelea Studio za +255 Global Radio akiambatana na Idara ya Habari ya klabu hiyo ndani ya Global Group kwenye ziara ya kikazi yenye lengo la kukuza na kudumisha mahusiano na idara ya habari.

 

“Hii ni mara yangu ya tatu kutembelea media houses Tanzania tangu niingie kwenye kazi hii, tumekuja kuwaeleza mashabiki wetu na Watanzania mambo ambayo Simba SC tumepanga kuyafanya.

 

“Viongozi wa Simba SC wataongea na uongozi wa Clatous Chama kuangalia namna ya kuongeza mkataba wake ambao unaisha Julai 2021, nimesikia Yanga SC wanasema watamchukua, pale atacheza na nani? Pasi za visigino atampa nani?


“Ili Chama aweze kucheza vizuri anahitaji timu inayomiliki mpira, akienda Yanga SC atachezaje? Kwanza hawana pesa ya kumnunua, mkataba wake ni dola milioni moja, Yanga wana hiyo pesa? Mashabiki wa Simba SC wasibabaishwe na propaganda za mitandaoni, viongozi wana uchungu na timu hawawezi kuruhusu aondoke," amesema.

 


12 COMMENTS:

  1. Ni kweli uongozi hauwezi kuruhusi aondoke lakini vipi kwa mchezaji mwenyewe akitaka kuondoka yaani asipende kuendelea kuichezea Simba?

    ReplyDelete
  2. Jamani msimu umeanza watu warudi kwenye usajili? Tucheze mpira, sio kila kukicha usajili

    ReplyDelete
  3. Manara hajui anachokizungumza. Kwani kule simba Chama anacheza na nani? Wachezaji anaocheza nao wametoka mbinguni au wapi? Maneno ya kipuuzi na yasiyokuwa na afya kabisa. Yanga inauwezo wa kumsajili mchezaji yoyote wa VPL na hata yeye mwenyewe Manara anaweza kusajiliwa kama Yanga wakiamua

    ReplyDelete
    Replies
    1. πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† usichekeshe imma mchezaji wa Azam tu shua boy mmeshindwa kuvunja mjakataba,etu mna hela. Danganyweni tu nahao wabaowadanganya

      Delete
    2. Tonombe Mukoko, Tuisika na Catinyos kati ya mmoja wao anaweza linganishwa na Shure boy? Sure ni mdogo sana hawakaribii hawa kwa lolote

      Delete
    3. Jidanganyeni wote mliotaja Ni mbulula mpaka sasa hakuna walichoonesha zaidi Yule kocha aliyewakimbia mkaenda kumwokota mserbia kawaingiza mkenge na kuawaachia gundu

      Delete
  4. Kwann mmeshndwa kumsajil sure boy na wakat mliambia day lake n million 120 lkn nyie mnatoa million 20

    ReplyDelete
  5. Yanga wameshindwa kumbakisha Morison ndio wamsajili Chama

    ReplyDelete
  6. Utopolo Hamna kitu paleπŸ‘‰πŸ‘‰ 4g hazijuwatisha sasa tutawapiga Kama vital 0 au zaidi " kumbukeni kipigo Cha mwaka 1977"

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mm nakumbuka kuna team ilfungwa 5 al ahly na week ilofuata ikafungwa 5 vita

      Delete
    2. Basi ww kiazi unasahau ushalishwa sita, unakumbuka plan ya kocha wa Simba Patrick nyumbani hutoki funga kwenu lkn nyumbani kwa mkapa hutoki na yote yakatimia tukabamiza wote wawili kwa mkapa na tukafuzu raundi inatofuata. Sasa ww ulipigwa na mnyama mpaka leo unaweweseka kufikia hpo wapi.

      Delete
  7. Tushafungwa tano bila hapa nyumbani kimataifa, tunaenda kumpigia mtu sita bila kwao na kumchomoa mashindanoni. Mpira ni mbinu na uwezo ww record zako zote ukifika matuta kimataifa out, kiazi weee Simba is the next other mmh! mdebwedo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic