January 7, 2019


Baada ya kupokea kipigo cha ambao 3-0 dhidi ya Azam FC juzi kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi huko Zanzibar, Katibu wa Tawi la Yanga, Kjitonyama, Shamte Ally, amesema mashindano hayo hayana mvuto.

Kwa mujibu wa Radio One, Ally ameeleza kuwa kwa mwaka huu kidogo kumekuwa hakuna ushindani wa maana kutokana na aina ya timu zilizopo hivi sasa.

Ameeleza hakuna timu ambazo zimetokea nje ya nchi zaidi ya Simba, Yanga na Azam FC ambazo walau zimeleta morali kwa mashabiki visiwani humo.

Katibu huyo amesema kutokuwepo kwa timu za nje kama KCCA kumedhorotesha ushindani wa maana kama ilivyokuwa mwaka jana na iliyopita.

Kiongozi Ally anaamini pia kitendo cha timu kama Yanga kupeleka kikosi cha pili ni uhalisia wa michuano kukosa hadhi kubwa kama yaliyopita.

4 COMMENTS:

  1. Kama mashindano hayana ushindani kwanini Yanga wamechezea kichapo cha paka mwizi? Mashindano hayana ushindani kuna timu yenye ushindani kama Simba na Azam kwenye ukanda wetu huu wa Africa kwa sasa? Kama Yanga walijua mashindano hayana ushindani kwanini walipeleka timu Zanzibar? Kiwe kikosi cha kwanza au cha pili kufungwa ni kufungwa ungwana ni kukubali matokeo.

    ReplyDelete
  2. matokeo si yameshapatikana sasa nani kasema Yanga B haijafungwa ?
    kama wewe unasema ile ndio Yanga A basi una matatizo makubwa sana !!

    ReplyDelete
  3. Hivi unapelekaje kikosi A kwenda kugombea mil 15? Hiyo mil 15 sihela ya kulipa mishahara ya wachezaji wa3 tu!!! Kwa level ya mpira wa Tz Yanga,simba,azam ndio timu kubwa huwezi kuzipambanisha zigombeee mil 15. Simba wamepeleka kikosi A kwenda kugombea mil 15 wakati wanamashindano ambayo wakishinda wanaingiza mabilioni ya hela. Erasto nyoni amepata majeraha wikiendi ijayo wanaanza klabu bingwa sifhani km walifikiri vzr. Hata kama ni mechi zakujiandaa na klabu bingwa huwezi kunidanganya kucheza na malindi au kmkm eti ndio maandalizi yakucheza na As Vita hapo wamepepesa macho

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maneno yote hayo ni kutokana na kufungwa 3G na azam. Wakati Simba ilipofungwa na Mashujaa na sisi kusema kuwa ni kikosi cha pili ndicho kilichofungwa, wenyewe mkatukejeli kuwa simba ni simba tu hakuna simba A wala simba B. Sasa leo Yanga B inatoka wapi?
      Pia, suala la mchezaji kuumia, anaweza kuumia hata akiwa mazoezini, hilo ni jambo la kawaida. Huwezi kuzuia mchezaji asiumie kwa kumuweka benchi. Pia, tambueni kuwa mpira ni vita, lolote linaweza kutokea ukiwa uwanjani. Sasa na wao wachezaji wakiweka akilini kwamba akicheza ataumia, ni nani atacheza? au mnadhani wao wenyewe hawajipendi?!
      Kingine, timu au wachezaji kazi yao kubwa ni kucheza mpira. Kila mashindano yanapotokea na uongozi kurudhia, ni wazi na ni lazima mchezaji akipangwa acheze. Hapo uongozi umeshapiga mahesabu ya ile zawadi ambayo ni M.15 na umeona kuwa ina faida kulingana na uendeshaji wa timu kwa muda wote huo.
      Vile vile huwezi kufananisha mashindano ya klabu bingwa na mashindano ya mapinduzi. Unapoyalinganisha, kwanza anza kutofautisha MUDA ambao mashindano hayo yanaendeshwa ndipo uangalie aina ya zawadi. Mashinda haya ya mapinduzi yanagharimu muda wa siku 13 tu hadi kumalizika, na zawadi yake ni M. 15. Je hayo ya klabu bingwa yanachukua muda gani? na gharama za maandalizi zinafanana na haya ya mapinduzi?.
      Jingine ni kwamba, msiponde tu kisa mmefungwa na huku Simba ikifanya vizuri Mapinduzi Cup. Mkikumbuka mwaka jana zawadi ilikuwa ni M. 10 kamili, na nyinyi mlipeleka timu kamili na huku mlikuwa katika mashindano ya shirikisho, je ile M. 10 ilikuwa kubwa kuliko hii 15?
      ACHENI MAMBO YA SIZITAKI MBICHI HIZI! HAPO MNALETA SABABU MAANA MMEONA MBELE NI KUGUMU.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic