UONGOZI wa Alliance FC umesema wataifuata KMC kwa tahadhari kubwa kutokana na ugumu wa Ligi ulivyo kwani kila timu inahitaji matokeo.
KMC watacheza kesho na Alliance Uwanja wa Uhuru ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili baada ya ule wa awali uliopigwa Nyamagana Alliance kubeba pointi tatu kwa ushindi wa mabao 2-1.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Alliance, Jackson Mwafulango amesema wanatambua timu ya KMC ni miongoni mwa timu zenye ushindani, hesabu zao ni kuwafuata kwa tahadhari.
"Tumejipanga kutafuta matokeo na tunajua kazi yetu kwa sasa ni kusambaza upendo ila haitawezekana kama tutakuwa na kiburi ni lazima tuwaheshimu wapinzani wetu na mwisho wa siku dakika tisini zitaamua," amesema Mwafulango.
Alliance imekuwa na matokeo chanya baada ya kuwa chini ya kocha Malale Hamsini ambaye ameiongoza katika michezo sita bila kupoteza na kuifanya iwe nafasi ya nane ikiwa na pointi 32.
0 COMMENTS:
Post a Comment