February 9, 2019


KIUNGO mchezeshaji mpya wa Yanga, Mohammed Issa ‘Banka’, rasmi anatarajiwa kuonekana uwanjani kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Bara baada ya kumaliza adhabu yake ya kifungo pamoja na kupewa kibali na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Banka alifungiwa na Kamati ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Zisizoruhusiwa Michezoni ya Kanda ya Tano Afrika (RADO) ambayo ilitoa hukumu ya kum­fungia mwaka mmoja baada ya kugundulika kutumia madawa hayo kwenye michuano ya Cecafa.

Kiungo huyo alisajiliwa na Yanga kwenye msimu huu wa ligi akitokea Mtibwa Sugar,  adhabu yake ilimalizka Al­hamisi rasmi na anatarajiwa kuanza kuvalia jezi ya kijani na njano mbele ya JKT Tanzania, Mkwakwani, Tanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Simba, Hafidh Saleh, amesema kiungo huyo rasmi ataonekana uwanjani katika mchezo wa kesho dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa.

“Mchezaji wetu Banka adhabu yake imekwisha na amepewa leseni na TFF hivyo ataanza kuitumikia timu yetu kesho katika mchezo wetu wa ligi dhidi ya JKT endapo mwalimu ataona inafaa kwani amefanya mazoezi pamoja na timu.

“Adhabu ya Banka ime­malizika katika kipin­di kizuri ambacho timu inamhitaji, kama unavyoona ratiba ilivyotubana ya ligi, wachezaji ushindani ni mkubwa,” amesema Saleh.

1 COMMENTS:

  1. Huyu njmchezaji wa Simba au Yanga? Akizungumza na Saleh Jembe Mratibu wa Simba Hapo Tu!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic