February 19, 2019


KOCHA msaidizi wa Azam FC, Juma Mwambusi amesema uongozi umekaa na wachezaji ili kujua kinachowakwamisha wasipate matokeo kwenye ligi katika michezo yao ya hivi karibuni.

Azam FC walianza kulazimisha sare mbele ya Alliance uwanja wa Chamazi kabla ya kusafiri na kupata sare mbele ya Lipuli uwanja wa Samora na kumalizia kwa kufungwa na Tazania Prisons bao 1-0 kabla ya leo kumenyana na Coastal Union, Mkwakwani.

Mwambusi amesema ni hali ambayo hawakutarajia kutokea kutokana na hesabu zao kubwa kukusanya pointi tatu kwenye michezo yao.

"Kama ambavyo imekuwa ikitokea kwa timu nyingine nasi pia tumepata matokeo ambayo si malengo, leo tunaingia kazini wachezaji wakiwa na ari mpya pamoja na morali kubwa.

"Tutashambulia na kujilinda kwa haraka ili tubaki kuwa salama, maana tulikaa kikao na wachezaji kujua kinachowasumbua, ushindani ni mkubwa tunahitaji sapoti,"  amesema Mwambusi.

Azam FC wapo nafasi ya pili kwenye ligi wamecheza michezo 23 na kujikusanyia pointi 49 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic