Meneja wa Chelsea, Maurizio Sarri amesema kuwa matokeo anayoyapata kwa sasa ni mara yake ya kwanza na anahofia kupata matokeo hayo mabaya.
"Nina mashaka makubwa na matkeo yangu na siyo mashabiki najua hali ambayo wanayo kwa sasa ila hich ndich kimetokea matokeo haya sio mazuri kwetu.
"Tumecheza vizuri ila wachezaji wangu wameshindwa kutumia nafasi ambaz wamezipata kwenye mchezo wetu, tuna kazi ya kuongeza umakini hasa kwa wachezaji wanapoingia ndani ya box maana hapo ndipo tulipozidiwa.
"Spidi na akili kwa wachezaji ni kitu muhimu ambacho kitaifanya timu kuwa bora, akili za mtu binafsi pamoja na uwezo wake mwenyewe akiwa ndani ya uwanja, kama ukishndwa kumiliki mpira inakuwa ngumu kupata ushindi," amesema.
Baada ya Chelsea kufungwa mabao 6-0 dhidi ya Manchester City kwenye Ligi Kuu England kumekuwa na presha ya kutaka kuondolewa kwa Sarri ndani ya kikosi hicho huku yeyey mwenyewe akisema hana mashaka na hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment