February 25, 2019




BAADA ya mabingwa watetezi wa kombe la FA kutolewa na kikosi cha KMC kwa mikwaju ya penalti 4-3 sasa hasira zao wanazielekeza kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Manungu kesho.

Katika mchezo wake wa FA, Uwanja wa Chamazi, ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 ndipo mwamuzi alipoamua zipigwe penalti na Mtibwa Sugar kuvuliwa ubingwa baada ya kushinda penalti 3-4.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa hakuna jambo la kufanya kwa kuwa mwamuzi wa mwisho kwenye mpira ni refa hivyo hesabu zake ni kwenye michezo inayofuata.

"Kwa sasa hakuna kingine cha kufanya zaidi ya kuwekeza nguvu zetu kwenye ligi ambayo bado inaendelea, waamuzi wanapaswa wawe makini kwani hii ni aibu kwetu.

"Mipango yetu ni kuona tunarejea kwenye ubora wetu na kila kitu kinawezekana endapo hakutakuwa na longolongo ili soka letu lipande, mchezo wetu ujao ni dhidi ya Coastal Union tunajipanga," amesema Katwila.

Mtibwa Sugar inashika nafasi 17 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza michezo 24.

2 COMMENTS:

  1. https://hellotaw.blogspot.com/

    ReplyDelete
  2. mpira hautaki maneno na majigambo katwila uende usomee ukocha acha mbwembwe utaadhirika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic