February 26, 2019


Kuelekea mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Lipuli dhidi ya Simba leo jioni huko Iringa, unaambiwa jina la Meddie Kagere ndiyo linaloongoza kutajwa zaidi.

Kagere amezidi kujizolea umaarufu Simba kutoka na mchango wake ndani ya kikosi hicho ambacho imekuwa na mwenendo mzuri hivi karibuni.

Straika huyo Mrundi aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia FC ya Kenya, aliisaidia Simba kupata mabao muhimu katika mechi dhidi ya Al Ahly ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kutokana na mwenendo wake, Kagere anapewa nafasi kubwa ya kufanya vema pia leo akiwa ugenini kwenye Uwanja wa Samora.

Licha ya kupewa nafasi, historia inaonesha Simba haijawahi kuifunga Lipuli tangu ipande daraja kucheza Ligi Kuu February 6 2017.

Licha ya kutoifunga, Lipuli nayo itakuwa inawakaribisha Simba ambayo hawajawi kuifunga kwenye Ligi tangu wapande kucheza ligi.

2 COMMENTS:

  1. Achana na hilo jina labda wamfanyie technicals wamtoe ila hamuachagi mtu salama huyo.

    ReplyDelete
  2. Achana na hilo jina labda wamfanyie technicals wamtoe ila hamuachagi mtu salama huyo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic