February 19, 2019



BADO rekodi za Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19 zinaendelea kuandikwa mpaka sasa ikiwa ni mzunguko wa pili na baadhi ya timu bado zipo mzunguko wa kwanza zinakamilisha viporo vyao.

Mpaka sasa viongozi wakubwa wa timu ambao ni manahodha wameonyeshwa kadi nyekundu ambazo ziliwafanya wakakosa michezo yao mitatu kwenye Ligi Kuu Bara.

John Bocco, nahodha wa Simba alikuwa wa kwanza kuonyeshwa kadi nyekundu msimu huu kwa upande wa manahodha kwenye mchezo wake wa kwanza kufuga mabao 2 msimu huu dhidi ya Mwadui uwanja wa Kambarage.

Bocco alionyeshwa kadi hiyo kwenye mchezo huo walioibuka na ushindi wa mabao 3-1 baada ya mwamuzi kutafsiri kitendo chake cha kumpiga kiwiko mchezaji wa Mwadui Revocatus Richard hali iliyopelekea mwamuzi kumuonyesha kadi nyekundu.


Pia nahodha wa Tanzania Prisons Laurian Mpalile naye pia alionyeshwa kadi ya nyekundu baada ya kuonyesha vitendo visivyo vya kinidhamu kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga.

Mchezo huo ulikamilika kwa Yanga kutoka kifua mbele kwa mabao 3-1 ulipiga kwenye Uwanja wa Sokoine.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic