NA SALEH ALLY
KAMA nilivyoanza katika makala zangu nyingine kwamba tunakubaliana Al Ahly au AS Vita Club ni timu zinazoizidi uwezo Simba au uwezo wao ni wa juu kama utazungumzia kiwango cha soka Tanzania.
Soka la DR Congo na lile la Misri kweli liko juu na nimefafanua kwenye makala yangu nyingine kwamba lazima tukubali na tujifunze.
Sawa, hili ni la kukubali lakini kitendo cha Simba kufungwa mabao 5-0 dhidi ya AS Vita, halafu mechi iliyofuata wakafungwa mabao 5-0 dhidi ya Al Ahly, inaonyesha kiasi gani kuna tatizo.
Wameingia kwenye kiwango kingine cha uchezaji soka ambacho kinawaonyesha walivyopungukiwa na wanatakiwa kubadilika kutokana na walipo.
Simba haiwezi kupiga hatua ikiwa na wachezaji wasio na nidhamu, wasio na uwezo mkubwa wa kujituma na malengo ya mafanikio.
Wachezaji ambao wamekuwa katika maisha ya kuamini ukubwa bila ya kujua kuna wakubwa zaidi yao.
Wachezaji wa Simba wameingia kwenye kashfa ya kwenda klabu usiku, kuonekana wamelewa huku wakijua wana mechi ya mashindano ya Kombe la SportPesa.
Walifanya hivyo wakiwa katika maandalizi ya mechi yao dhidi ya Al Ahly. Michuano ya SportPesa Super Cup ilikuwa ni maandalizi ya mechi hiyo.
Hawakuwa makini, walionyesha hata maandalizi yenyewe hawakuwa makini. Sasa vipi wangeweza kushinda dhidi ya timu inayowazidi kiwango tena kwa kiwango kikubwa.
Suala la Al Ahly kuizidi Simba kiwango linaweza kuwa hadithi mpya ya kuisikia leo? Sote tunalijua na kama unakutana na anayekuzidi kiwango lazima maandalizi yako yawe tofauti na mengine.
Sasa Simba walikuwa wametoka katika kipigo kikubwa cha mabao 5-0 dhidi ya AS Vita Club ya DR Congo, halafu waliporejea nyumbani wakatumia kigezo cha "soka ndivyo lilivyo" kuendelea kufanya madudu.
Ukweli kuna wachezaji ndani ya Simba ambao hawana kiwango cha kuichezea Simba si kwa maana ya uwanjani, badala yake ni elimu ya uelewa wa kile wanachokitumia.
Niliandika makala kueleza namna ambavyo wachezaji wa Simba wanapaswa kuelewa angalau thamani ya jezi wanayoivaa badala ya kuona kama vile wao ndio wanaisaidia Simba.
Mtu anaweza kuwa anakuzidi uwezo wa kitu fulani mnachoshindania. Lakini maandalizi mazuri, juhudi za kutosha zinapunguza pengo la ubora kati yako na yake na mwisho kufanikiwa.
Haiwezekani Al Ahly wakawa katika maandalizi makini wakati wanajiandaa kukutana na Simba, halafu Simba wakawa katika maandalizi ya tia maji tia maji.
Kuna mtu anasema wachezaji wanavimbishwa vichwa na vyombo vya habari, jambo ambalo naona upo uwezekano wa asilimia 10 tu lakini 90 utakuwa ni upuuzi wa wachezaji wenyewe, hasa kama ni kweli.
Mchezaji amefunga mabao mawili, vipi asisifiwe na kinachoongelewa ni ligi ya nyumbani. Lakini kama ni michezo ya kimataifa, wanashinda mechi dhidi ya JS Saoura tena kwa mabao 3-0, vipi usiwasifie?
Kuwasifia ndani yake kuna kuwakumbusha. Hapa ningependa zaidi nizungumzie Gazeti la Championi au Spoti Xtra na si mengine. Juhudi kubwa za kuwakosoa na kuwasifia wachezaji wa Tanzania na wageni walio hapa zinafanyika.
Hatuwezi kuwajenga kwa kuwaponda tu, lakini kukubaliana na ukweli wanapofanya vizuri. Lakini wakifanya vibaya waambiwe kama ambavyo inafanyika sasa na ilifanyika wakati wa AS Vita Club lakini inaonekana wao hawakulifanyia kazi hilo.
Sifa kuu ya watu wa Kaskazini mwa Afrika ni nidhamu katika soka. Tunajua, mchezaji baada ya maandalizi ya mwanzo wa msimu anatakiwa kujitunza na hasa kujiepusha na mambo ya starehe.
Wenzetu wana sifa ya kujitunza sababu wana nidhamu na wanajitambua. Wachezaji wetu kiwango ni duni kwa kuwa hawajitunzi maana yake hawajitambui.
Kutakuwa na mengi sana ya kuitengeneza Simba na funzo hili litaenda kwa wengine pia wakipata nafasi katika kiwango hiki.
Kiukweli wachezaji wa Simba wana sehemu kubwa ya kuwajibika katika hili. Maana pamoja na kuzidiwa bado walionekana si wanaotaka kujitoa. Simba imeonyeshwa inapaswa kuwa na uamuzi mgumu, sahihi usio na hofu ya lawama.
Kwani shida iko wapi..Si Chelsea juzi kapigwa 4.Halafu Yanga kuwa wanaiambia Simba LA kufanya sio vema..Yanga Nafasi ya kucheza klabu bingwa Afrika wamekuwa wanafika wapi.Wanailaumu Simba kufungwa goli 5 na timu iliyochukua ubingwa wa CAF Mara nane wakati wao Mwaka Jana walikuwa wanapigwa 3 na Gor Mahia..Acheni unafiki wenu...Saleh unaweza Fanya bora zaidi ya upuuzi huu..
ReplyDeleteWangeshinda Simba SAA hii Salehe angekuwa anaandika habari za viporo kurudisha soka LA Tz
ReplyDeleteNaungana na Saleh Jembe,Simba kuna tatizo. Cha kushangaza ni jinsi pale unapoona wachezaji wa wanaposhindwa angalau kuonesha jitihada binafsi ya kupamba angalau ahisi kunauwezekano wakuwa ataonenaka na vilabu vengine kwa maslahi yake mapana zaidi ya baadae. Unajua kwa mtu au taasisi kufanya kosa la mara ya kwanza watu huchukulia kuwa ni kuteleza lakini kwa mtu yuleyule kurejea kutenda kosa lile tena kwa hali ya hovyo kabisa kuliko mara ya kwanza huo unaitwa ni uzembe na adhabu ya mzembe ni kuwajibishwa hakuna msalie mtume au baba yesu asifuwe, kusifia uzembe? Kwa wenzetu wenye kufanya kazi zao kwa speed ya treni ya umeme basi kosa la kwanza tu ukifanya linaangaliwa lina uzito wa aina gani mazali umeajiriwa kufanya kazi kama professional utawajibishwa tu na ndio maana wa Algeria wa js Soura waliungalia mchezo wa timu yao na Simba wakagundua kocha wao alipaswa kuwajibika na kweli wakamtimua na badala ya hapo Saoura sasa wamepata nguvu mpya. Sisi watanzania tumezoea kufanya kazi kwa kasi ya mwendo wa konokono kwa hii dunia ya sasa kamwe hatutafika tunapotaka kwenda.
ReplyDeleteHakika, naunga mkono, Simba ndani mle kutakuwa na tatizo tena kubwa sana. Tena kwa mtazamo wangu nahisi tatizo ni kocha, maana mara nyingi wachezaji wa Simba wakipishana na kocha tu, huwa wanacheza kukamilisha ratiba tu ili wamkomoe kocha kwa lengo la kumfukuzisha kocha kazi.
ReplyDeleteSasa hili inabidi liangaliwe, itakuwa kocha haendi sawa na wachezaji. Uongozi ujaribu kukaa na wachezaji pekee nje ya benchi la ufundi, watambue kuna changamoto gani inayoendelea.
tatizo la simba ni benchi zima la ufundi kuanzia kocha na wasaidizi wake wote sababu hawafanyi tathmini ya timu watakayokuja kucheza nayo na kupanga mbinu za jinsi ya kuucheza mcheco ulio mbele yao. wao wanafika uwanjani na kucheza bila kujua ni style gani timu pinzani inatumia na ni wachezaji gari hatari wa kuwaangalia na kuwapangia wachezaji wa kuwabana ili wasicheze kama wanavyotaka. nilikua nafatilia ile mechi na kumsikiliza vizuri yule mtangazaji mmisry akiwachambua wachezaji wa simba mmoja mmoja yaani anayo historia ya wachezaji wote wa simba na club walizotokea pamoja na nchi zao na mafanikio yao katika timu zao za Taifa na hata club !! jamaa walikua wanajua vipi wambane okwi na kagere pia chama na pia uzito wa beki wawa walikua wanaujua vizuri na kupenyeza mipira kwake !! tunatakiwa na sisi kufanya hivyo lazima tufatilie mechi za wapinzani kwa umakini na kujua nini tutafanya tutakapokutana nao . Al Ahly watakapokuja Tz watacheza vingine maana wanajua kua Simba watabadilika kwa kua wapo nyumbani na wana sapoti ya washangiliaji hivyo simba lazima washambulie kwa nguvu tokea dakika ya kwanza huku wakiwa makini na kuwabana wachezaji kama Ali A maaloul, Junior Ajayi na Hussein El Shahat. huy Hussein El Shahat ndie hatari Zaidi anayefight dakika zote na ndiye aliyeifikisha club ya Al Ayn ya Emirate final ya kombe la dunia la vilabu na kufungwa na Real Madrid mchezo wa fainali . tukimbana huyu tutakua tumepunguza nguvu ya Al Ahly kwa karibu ya asilimia 35
ReplyDelete