February 22, 2019


MSHAMBULIAJI wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi amesema kuwa hakuna atakayebaki salama mbele yao kwa kuhakikisha wanashinda mechi zao zote ili waweze kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Simba ina pointi 45, wakizidiwa pointi tano na Azam FC inayoshika nafasi ya pili baada ya kuicharaza leo mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Okwi alisema malengo yao ni kuhakikisha wanafanikiwa kutetea ubingwa wao kwa kushinda kila mchezo uliopo mbele yao ukiwemo wa leo.

“Sasa hivi tunaangalia mechi za mbele ikiwemo baada ya Azam, sisi hatuangalii zimebaki mechi ngapi, tunaangalia kushinda kila mechi baada ya nyingine kwa sababu tunachokitaka ni kupata pointi tatu.

“Kuifunga Yanga ni ushindi kama ulivyo ushindi wa kawaida, ndiyo ni derby lakini hilo lishapita na limebaki kwenye historia ila kwa kuwa tumemfunga, aliyekuwa juu yetu imeongeza kitu maana malengo ni kuchukua ubingwa,” alisema Okwi.

Upande wa afya yake Okwi amepona na yupo fiti baada ya kusumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu wakati beki wa kati Juuko Murshid anasumbuliwa na maumivu ya ugoko.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema: “Okwi ana asilimia 100 ya kucheza hivi sasa, Juuko bado hajawa fiti na uwezekano wa kuwepo kikosini ni mdogo.” 

Aidha, Rweyemamu alisema mshambuliaji Meddie Kagere anatarajiwa kuwepo kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kadi tatu za njano.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic