February 22, 2019



NAHODHA wa Simba, John Bocco leo amewaongoza wachezaji wenzake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Mkapa.

Mchezo huu ambao ni kiporo cha mzunguko wa kwanza Simba wanafanikiwa kukimalizia vizuri licha ya ushindani walioupata kutoka kwa wapinzani wao Azam FC.

Bao la kwanza kwa Simba lilipachikwa kimiani na Meddie Kagere dakika ya nne baada ya mshambuliaji Emanuel Okwi kuachia shuti kali lililogonga mwamba na kurejea uwanjni kisha likakutana na kichwa cha Kagere.

Iliwalazimu Simba kusubiri mpaka dakika ya 39 kupachika bao la ushindi baada ya Simba kupata kona iliyoanzishwa na Okwi kisha akampa mzee wa kumwanga na kumimina maji Zana Coulibaly aliyeachia majalo yalikutana na kichwa cha Bocco.

Mpaka dakika 45 za mwanzo zinakamilika Simba walikuwa mbele kwa mabao 2 bila na kurejea kipindi cha pili ambapo tena iliwalazimu Simba kusubiri mpaka dakika ya 78 kupachika bao la tatu ambalo lilianzia kwa Clatous Chama kabla ya kumkuta Kagere ambaye alibabatiza mpira kisha akauzamisha nyavuni kwa mguu wake wa kulia.

Baada ya bao hilo alielekea kwenye goli akiwa na Dilunga, Zana kuutafuta mpira ulipopotelea.

Bao pekee la Azam FC walilipata kupitia kwa Frank Domayo aliyegonga bonge moja la shuti na kuingia ndani na ukarejea tena uwanjani akimalizia pasi ya Donald Ngoma. 

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 45 ikiwa imecheza michezo 18 inabakiz pointi tano kuifikia Azam FC ambayo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 50 huku mlima wa kuifikia Yanga ukibaki pointi 16.

5 COMMENTS:

  1. Simba wamebadilika hawaonekani tena kuremba bali wanachoangalia ni point tatu. Kagere na okwi hawa ni watu wa vita unawaona kabisa jinsi wanavyopambana,jinsi walivyo na hasira ya kufunga misili ya mtu anaepambana na watu wanaomzuia kuingia ndani ya nyumba yake. Hata Boko anaonekana kutulia sasa aendelee kujiweka sawa kwani Boko ni mchezaji mkubwa anaeweza kufanya mambo makubwa wakati wowote ndani ya dakika tisini za mchezo. Hao wanaosema kagere mzee nadhani wao ndio waliozeeka akili hazifanyi kazi tena. Nataka Adam Salamba amtizame sana kagere na sio kumtizama tu bali kuwa karibu nae na kufanya mazungumzo nae na akipata nafasi Adam Salamba ya kuzungumza na kagere basi amuulize kwanini kula kukicha anazidi kuwa bora? Amuulize na tena kwanini wewe kagere mechi inaanza mpaka inamalizika unahaha kutaka kupachika magoli kana kwamba hajawahi kufunga bao katika maisha yake tangu aanze kucheza mpira?. Salamba akipata nafasi na amuize tena kagere inakuwaje muheshimiwa kagere licha ya kujaliwa mwili ulioshiba lakini ni mwepesi na mwenye kasi zaidi kuliko kinda Salamba,nini siri yake?Nnaimani salamba anamengi ya kujifunza hata kuiga kutoka kwa mtu kama kagere ikiwa kama yeye mwenyewe Salamba yupo tayari kujifunza na nnaimani atanufaika sana.

    ReplyDelete
  2. Kweli tangu Simba walipoacha kulemba na magoli yameongezeza...Walipocheza na African Lyon walitumia pasi ndefu..Na Jana pia pasi ndefu zilionekana na zimezaa matunda...Tunapenda pasi fupi zinaleta raha katika Mpira..ila mwisho wa Siku kinachopendwa ni magoli!!

    ReplyDelete
  3. Simba Sasa Ni Mwendo Mdundo No Show Game Magori Mengi Japo Bado Hayatoshi Nataka Tumpe Mtu 5 Bocco, Kagere, Okwi Mna Tisha Salamba Jifunze Kwao

    ReplyDelete
  4. Kiujumla mpira ulipoanza nilidhani kiwango kimeshuka, ila kwa kadri dakika zilipozidi kwenda kasi ya Simba ikawa inazidi kuongezeka. Na ikafikia kuendelea kuiona Simba ambayo ni tofauti kabisa. Heko kwa benchi la ufundi kwa mabadiliko waliyoyaingiza, naamini yamesaidia sana. Na pia heko kwa wachezaji kwakuwa naamini wamejitambua sasa, hawachezi rojorojo kwasasa, wanapambana. Waendelee kukumbuka kuwa ile ni ajira ambayo wameichagua wao wenyewe, hivyo wanatakiwa kupambana ili kujitengenezea mazingira mazuri kwa ajira yao, ili ifikie wakati wahitajike kwa timu kubwa hata barani Ulaya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic