February 22, 2019




CHELSEA imezuiwa kufanya usajili wa wachezaji kwa misimu miwili  ya usajili kwenye dirisha dogo na kubwa baada ya kubainika kukiuka taratibu za usajili za Shrikikosho la Mpira Duniani (FIFA).
Chelsea imehukumiwa kwa kosa la kufanya usajili kwa watoto  walio chini ya miaka 18 ambayo ni kinyume cha sheria namba 19.
FIFA imeipa klabu siku 90 kukamilisha  masuala ya yao ya usajili kwa wachezaji ambao wamemwaga wino kwenda sawa na taratibu ambazo zimewkekwa.
Uongozi wa Chelsea umesema kuwa wanachukua hatua ya kukata rufaa kwa ajili ya maamuzi hayo kupinga hukumu hiyo.
Rufaa hiyo itasikilizwa na kamati ya rufaa ya FIFA ila timu ina nafasi ya kukata rufaa kwenye mahakama ya haki za michezo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic