February 21, 2019





KIJANA Simon Muray ambaye ni shabiki wa klabu ya Simba ametumia siku mbili kutoka Manyara kuja Dar es Salaam kufuata mamilioni ya Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya M-Bet baada ya kuibuka mshindi wa Perfect 12.

Muray alishinda Perfect 12 ya Februari 17 na kuondoka na kiasi cha milioni 81 baada ya kubashiri kwa usahihi timu 12 ambazo aliweka kwenye mkeka wake.

Mshindi huyo ni wa pili kwa hivi karibuni kuvuna mamilioni ya Perfect 12 ya M-Bet baada ya Frank Kayombo kushinda milioni 188.

Akizungumzia juu ya ushindi wake, Muray amesema: "Hadi mnaniona nimefika hapa Dar nimetumia siku mbili njiani nikitoka Manyara, ambapo nafanya masuala ya kilimo.


"Nimekuwa nikicheza kwa miezi miwili sasa, nilikuwa nikichanganya normal na hii Perfect 12. Wakati ndiyo nimepigiwa simu nikiambiwa ndiyo mshindi nikajua ni watu matapeli tu lakini baada ya kuelekezwa sana nikaamini kweli nimeshinda.

"Mimi ni shabiki wa Simba pamoja na Real Madrid, baada ya kushinda sasa hizi fedha nitazitumia katika mambo yangu ya msingi ikiwemo kuendeleza kilimo, kusomesha watoto wangu kwenye shule za kimataifa," amesema Muray.

Simoni ameshinda dau la 81,097, 540 la Perfect 12.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic