February 21, 2019



KOCHA Mwinyi Zahera wa Yanga, jana amevunja mwiko kwenye uwanja wa CCM Kirumba baada kushindwa kupata matokeo kwenye mechi mbili walicheza.

Mara ya kwanza msimu wa 2015/16 ilipoteza kwa kuchapwa mabao 1-0 na mara ya pili msimu wa 2017/18 ikanyooshwa 2-0.

Jana Yanga ilishinda mabao 2-1 na kufikisha pointi 61.Zahera amefuta ufalme wa Mbao kuitesa na imepigwa nje ndani kwani mchezo wa mzunguko wa kwanza ilifungwa mabao 2-0 Uwanja wa Mkapa.

 Kwa ushindi wa Yanga iliyocheza michezo 25 imeizidi Simba inayokula viporo kwa pointi 19.

Simba ina pointi 42 ipo nafasi ya tatu imebebeshwa mzigo wa pointi 19 ili iweze kuishusha Yanga.

2 COMMENTS:

  1. Kuvuna points kutoka kwa klabu namba moja barani Africa Alahly na kuchukua points kutoka kwa wao wenyewe Yanga haukuwa mzigo mzito kwa Simba vipi hao wengine? Sijui kama yanga angeifunga Simba kelele zingekuwa za kiasi gani?

    ReplyDelete
  2. wasubiri mwisho wa april waongee

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic