February 27, 2019


Licha ya kuifunga Lipuli FC jana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa bao 3-1. Uongozi wa Stand United umetuma salaam mapema za maangamizi kwa wekundu hao wa Kariakoo.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Stand, Athuman Bilal 'Bilo', amewataka Simba kujiandaa vema kisaikolojia wakienda kucheza na timu inayobutua mpira.

Bilo amewaambia Simba wao kama ni timu ya bilioni 1.3, wao hawajali hilo na watahakikisha wanawachukulia alama tatu kama walivyofanya kwa Yanga.

"Nawaambia kabisa Simba kuwa tutakapokutana nao Machi 3 wajiandae kushangazwa na wachezaji wetu wa ajabu, tutakutana Kambarage na tutawaonesha kuwa hatukubahatisha kwa Yanga", alisema.

Stand wanaenda kucheza na Simba Machi 3 kwenye uwanja wao wa nyumbani wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.



5 COMMENTS:

  1. Dah! Watu Wengine Bwana Wanajua Kulopoka Nani Ajitayarishe Kisaikolojia Kati Ya Simba Inayo Ongoza Kwa Viporo Lakini Imefunga Goal 41 Na Point 48,kuwazidi Wao Walio Tangulia Mech Na Iliyo Nafasi Ya Pili Kwa Tofauti Ya Point 1 Hatua Ya Makundi Club Bingwa Africa Na Iliyo Ifunga Ally Ahly Club Bora Africa Na Stand Iliyo Cheza Mech Zaidi 25 Na Ipo Nyuma Kwa Pointi Nyingi Na Magoli Kuliko Simba Imepoteza Mechi Kibao Na Droo Kibao Kuliko Simba Inaonekana Huyo Hajui Kusoma Takwimu

    ReplyDelete
  2. Hata Matola alisema hivuo!au Bill hakulijua hilo..Yanga ni Yanga na Simba ni Simba

    ReplyDelete
  3. Brother Bilo angalia usije haribu kibarua chako.Maana unaweza kufungwa 5-0 itakuwa ni tatizo kwako.Usilinganishe Yanga kwa Simba

    ReplyDelete
  4. Matola alitamka kama hayo na baadae kaishia kuwa wachezaji wake walifanya makosa

    ReplyDelete
  5. Yeyote anayejigamba kumpigisha magoti mnyama, kwanza wakamuulize yanga, Azam na Lipuli

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic