February 27, 2019


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema malengo yake ni kuiweka timu kileleni mpaka msimu wa Ligi Kuu Bara 2018/19 unamalizika.

Mpaka sasa Yanga inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 61 dhidi ya Azam iliyo na 50 huku Simba wakiwa na 48.

Akili ambayo Zahera ameeleza kuja nayo ni kuhakikisha wanashinda mechi za mikoani ambazo wamekuwa wakipata wakati mgumu kuchukua pointi tatu.

Ameongeza kwa kueleza kuwa wachezaji wake wanapaswa pia kuwa na akili ya kucheza ikiwemo kupiga pasi za kuwapoteza wapinzani haswa wanapokamiwa dimbani.

Kocha huyo mwenye maneno mengi, amewataka pia wachezaji wake kutotumia nguvu nyingi uwanjani bali akili, jambo ambalo halitosababisha kuchoka mapema.

"Malengo yetu ni kuchukua ubingwa, nitakikisha wachezaji wanatumia akili wakiwa uwanjani na si kukimbia hovyo sababu watachoka, tutapambana kushinda mechi zetu zijazo haswa za ugenini" alisema.

3 COMMENTS:

  1. Amesha Chelewa Kuwaelekeza Wachezaji Wake Kutotumia Nguvu Uwanjani Nimeona Uchezaji Wa Yanga Hasa Beki Zimekuwa Zikitumia Nguvu Kukaba Utadhania Wako Ulingoni Tofauti Kabisa Na Watalaam Wa Mpira Beki Za Simba Kama Tshabalala, Nyoni, Wawa Na Zana Wanatumia Akili Kunyang'anya Mpira Kuja Mbele Pale Ni Wazee Wa Mipango Akili Kwa Sana Utakubaliana Nami Kama Uliangalia Magol Ya Simba Jana Dhidi Ya Lipuli Faulo Ya Kwanza Na Ya 3 Zilizo Zaa Magoli Yaliyo Fungwa Na Chama Na Hata Gol La 3 Mk 14 Akili Tu Wala Sio Nguvu Kama Shambani

    ReplyDelete
  2. Maumivu gani hayo. Wacheni porojo halafu munaangukia ukingoni. Makucha ya Simba makali kuliko uwembe. Munafanya kejeli halafu mnalia. Hata Plujin nae si pia alijigamba na si umemuona kilichomfika. Tieni nywele sabuni mungoje zamu yenu

    ReplyDelete
  3. Anazungumzia kushinda mechi zote alizobakiza!, sasa na Simba ashinde mechi zake zote zilizobakia, hilo kombe atalichukua kwa kigezo gani!, labda wao Yanga wawe wanacheza mechi 41 na Simba inaishia 38. Hapo hadi sasa Zahera anatakiwa kuiombea mabaya Simba tu, hana ujanja hadi dakika hii. Azam anamsubiri kule.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic