February 13, 2019


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia, amewapongeza Simba kwa kufanikisha kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly katika Uwanja wa Taifa jana.

Karia ameeleza walichokifanya Simba ni kitu kikubwa kwa taifa kwani wanazidi kuitangaza nchi vizuri na kuzidi kujiwekea matumaini ya kufanya vizuri zaidi usoni.

Rais huyo pia amezidi kuwatakia kheri Simba katika maandalizi ya mechi zijazo za kimataifa ili wazidi kufanya kweli na kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Aidha, Karia amezitaka timu zingine pia zijitume vizuri ili ziwe zinaiwakilisha Tanzania kimataifa kwasababu akisema wao kama TFF huwa wanaziunga mkono timu zote zinazowakilisha nchi.

"Nawapongea Simba wamefanya vizuri, wazidi kujipanga vilivyo kwa mechi zingine zilizosalia, naimani watafanya vizuri. Sisi kama TFF jukumu letu ni kuzipa sapoti timu zote zinazowakilisha nchi, hivyo wengine wanapaswa kupambana ili waipe uwakilishi mzuri Tanzania" alisema.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic