February 13, 2019


Na George Mganga

Mchezaji wa zamani wa Yanga, Bakali Malima maarufu kama Jembe Ulaya, amewahadaa Simba kwa kusema licha ya kuibuka na ushindi dhidi ya Al Ahly, bado hawana asilimia 100 ya kuibuka na ushindi dhidi ya Yanga Jumamosi ya wiki hii.

Kwa mujibu wa Radio One, Malima ambaye aliwahi kung'ara na kikosi cha Yanga miaka ya zamani, anaamini mechi ya watani wa jadi ina upekee wa kiana yake, na si rahisi kutabirika kama ambavyo wengi wanaichukulia Yanga hivi sasa.

Kitendo cha Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana ukiwa ni mchezo wa kundi D, hauchukulii kama sababu ya wao kuifunga Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

"Unajua mechi hizi za watani wa jadi huwa hazitabiriki kirahisi kama wengi wanavyodhania, kitendo cha Simba kuwafunga Al Ahly haitoi taswira kuwa watapata matokeo mbele ya Yanga Jumamosi, naimani Yanga inaweza onyesha maajabu" alisema.

Yanga akiwa mwenyeji wa mechi hiyo, atakuwa anacheza na Simba huku mechi ya raundi ya kwanza iliyochezwa mwaka jana timu hizo zilimaliza dakika 90 kwa suluhu tasa ya bila kufungana.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic