February 23, 2019



KESHO jumapili kikosi cha Namungo kitaikaribisha Yanga uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi kwenye mchezo wa kombe la FA huku vita kubwa ikiwa ni kwa kutafuta ushindi.

Timu zote mbili kwenye ligi ni vinara na zinapeta kutokana na uimara wao hali itakayoongeza ushindani.

Yanga wanaongoza Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 61 wakiwa wamefunga mabao 42 hali ambayo inawafanya mashabiki waamini wataibuka na ushindi kwenye mchezo wao huo.

Namungo nao wanajivunia nafasi ambayo wapo kwani kwenye Ligi Daraja la kwanza wakiwa kundi A wao ni vinara wa ligi hiyo.

Namungo wanaongoza kundi A wakiwa na pointi 28 na mpaka sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja katika michezo 14 na wamefunga mabao 29.

Pia Namungo wana rekodi ya kutopoteza michezo yao ya kirafiki kwa timu zote zilizo nafasi ya tatu ambazo ni Yanga, Simba na Azam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic