March 31, 2019


Alichokiandika Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla kuhusiana na Mchekeshaji, Pierre Liquid.

Andiko hili limekuja kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kusema wanahahabari waache kumpa kiumbele Pierre sababu ya ulevi


It’s ok! It’s ok! It’s ok, very ok kwa Pierre Liquid kufanya anachofanya na kufurahisha wanaoona ‘anachekesha’. 

Nchi haiwezi kujengwa na watu wanaofanya mambo magumu magumu pekee. Kila mmoja wetu anafanya sehemu yake. Pierre anatuchekesha na kutukumbusha kufurahia maisha tunapopata nafasi, haswa tunapotoka kufanya hayo mambo yetu magumu magumu!

Jamani maisha ni magumu, yana mitihani mingi na ni mafupi sana. Katika kuleta furaha na shangwe kwenye maisha ndiyo maana ‘wachekeshaji’ wakapata ajira! Wengine tusome udaktari, uhandisi na tufanye uvumbuzi na utatuzi wa changamoto na wengine watutetemeshe, watuvuruge akili, watupe raha na furaha, watuchekeshe, siku zisogee.

Maisha ndiyo haya haya! Zaidi ya yote, Pierre ni mtu huru kwenye nchi yake. Tunapaswa kuulinda uhuru wa Pierre kama ambavyo Katiba ya nchi yetu inavyoelekeza. Let him be. Tumuache apate riziki yake. 

Mungu anajua zaidi kwa nini hatukumjua miaka 5 iliyopita na kwa nini sasa anazua mjadala. Hata kwa mimi binafsi, Mungu anajua zaidi kwa nini sikuwa Waziri miaka mitano iliyopita, na leo ni Waziri. Mungu anatupangia maisha yetu. Anatugawia mafungu yetu.

Pengine hii inaweza kuwa sababu ya Pierre kuwa mtu bora zaidi leo kuliko ile siku aliyopiga ukelele wa raha na kubembea pale Liquid! Pengine hii ndiyo nyota yake ya jaha. Kwa hakika, Pierre atabaki kuwa juu! Pierre atabaki kuwa kileleni! Everebade sey yeeh! #HK



3 COMMENTS:

  1. Naungana na Muheshimiwa Paul Makonda kwa asilimia mia moja 100% kuwa piere tukukuzwe kwa uchekeshaji wake lakini suala la kutukuzwa kwa ulevi kama taifa ambalo asilimia kubwa ya wananchi wake ni vijana basi hii ni jitihada za makusudi za kujenga Taifa la walevi. Muheshimiwa Kigwangala ni mtaalam wa Afya bila shaka angetumia taaluma yake ya afya kueleza athari za pombe kiafya kwa mwanadamu. Makonda ni mkuu wa kamati ya Amani na usalama kwa wananchi wake wa mkoa wa Dareslaam na amezungukwa na wadau au washauri wa kada mbali mbali kama vile Mashehe,Mapadri,Wazazi,
    Wazee,Makamanda wa polisi,Wataalam wa fya nakadhalika nakadhalika. Kwa kifupi Majukumu ya Makonda kama mkuu wa mkoa wenye ushawishi mkubwa kwa maisha ya watanzania ni mazito na anapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote kwa kile atakachokikemea ambacho kina kila dalili ya kujenga jamii njema.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic