March 9, 2019


BAADA ya droo ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kuonyesha kwamba Alliance watacheza na Yanga, Kocha Mkuu wa Alliance, Malale Hamsini amesema amefurahi kukutana tena na Yanga.

Alliance katika mchezo uliopita dhidi ya Yanga ambao ulikuwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ilikubali kipigo cha bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 

Hamsini alisema kuwa kupangwa na kucheza na timu kubwa kama Yanga kunawajengea uzoefu zaidi lakini nia yao ni kupata ushindi kwa safari hii kwani walishapoteza mara ya pili dhidi yao.

“Mara ya kwanza tumefungwa pale Taifa mabao matatu, tukaja Mwanza tukafungwa pia bao moja, unaona ni jinsi gani tunapiga hatua, safari hii tunahitaji kupata ushindi japo ni vigumu kuupata kutokana na uwezo walionao wachezaji wa Yanga ambao wengi ni wazoefu,” alisema Hamsini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic