MAJALIWA AONESHA JEURI YA PESA, ALIPIA VIINGILIO, ATOA BASI JIPYA
Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewalipia viingilio mashabiki wa soka katika jimbo hilo kwaajili ya kushuhudia mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza kati ya Namungo FC dhidi Majimaji FC.
Mchezo huo muhimu kwa kila timu katika mbio za kupanda daraja, utapigwa leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani humo.
Mchezo huo utaambatana na hafla ya Namungo FC kukabidhiwa basi jipya ambalo limetolewa na wadau wa soka mkoani Lindi kwa kushirikiana na Mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa.
Kukabidhiwa kwa basi hilo (pichani) sasa kunaifanya Namungo FC sasa iwe na mabasi mawili.
CHANZO: AZAM TV
0 COMMENTS:
Post a Comment