March 9, 2019



KIKOSI cha Simba mpaka sasa kimataifa kimeshuka Uwanjani mara nane kuanzia hatua ya awali msimu huu.

Katika michezo hiyo nane, Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mechi tano na imenyooshwa kwenye michezo mitatu.

Ushindi waliopata Simba ni dhidi ya Mbabane Swallow ambao waliwapiga nje ndani kwa jumla ya mabao 8-1, Nkana FC waliwafunga jumla ya mabao 3-1, Al Ahly waliwafunga bao 1-0 na JS Saoura iliwafunga mabao 3-0.

Simba wamefungwa dhidi ya Nkana FC 2-1, AS Vita 5-0 na Al Ahly 5-0 zote wakiwa ugenini.

Mpaka sasa Simba imefungwa jumla ya mabao 13 kimataifa huku wakifunga jumla ya mabao 16 kimataifa na mshambuliaji mwenye mabao mengi ni Meddie Kagere ambaye amefunga mabao 6 kimataifa.

Leo Simba itakuwa kazini nchini Algeria kumenyana na JS Saoura mchezo ambao utakuwa na ushindani kutokana na kila timu kupiga hesabu za kutinga robo fainali.

Kwa sasa kwenye kundi D ambalo wapo Al Ahly ya Misri ni vinara wakiwa na pointi saba huku Simba wakiwa nafasi ya pili baada ya kujikusanyia pointi sita.

Wapinzani wao wa leo, JS Saoura wanashika nafasi ya tatu wakiwa wamekusanya pointi tano wanafuatiwa na AS Vita ya Congo ambao wana pointi nne kibindoni.

3 COMMENTS:

  1. SIMBA HAIKUFUNGWA NA NKANA RANGERS UONGO UONGO UONGO MTUPU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inawezekana ni kweli Simba haikufungwa na Nkana Rangers ya huko kijijini kwenu lakini ukweli unabaki pale pale kwamba Simba ilifungwa 2-1 na Nkana FC mjini Kitwe.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic