March 26, 2019



UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa wana imani kubwa ya kufanya vizuri kwenye hatua ya robo fainali kwenye mchezo wao wa Ijumaa dhidi ya Kagera Sugar ambao ni wa kombe la Shirikisho pamoja na ule wa ligi utakaochezwa April 3 Uwanja wa Nyamagana Mwanza.

Mratibu wa Azam FC, Philipo Alando amesema kuwa wamejipanga kiasi cha kutosha kutokana na uimara wa kikosi chao pamoja na matokeo chanya ambayo waliyapata kwenye mechi zao za karibuni.

"Tupo tayari kiushindani  na tunatambua kwamba tunacheza nao mchezo wa shirikisho pia tutakutana kwenye mchezo wa ligi hivyo sio kazi nyepesi ambayo tunakwenda kuifanya kutokana na ubora wa wapinzani wetu kwani tunawaheshimu na tunajua ubora wao," amesema Alando.

Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa hawana hofu na Azam kwani ligi ilivyo kwa sasa ina ushindani mkubwa na mchezo wao wa Shirikisho walishajiaanda tangu mapema.

"Maandalizi yetu yalianza mapema kwenye mchezo wetu wa shirikisho, kwa upande wa ligi kwa sasa hakuna cha kupoteza ni lazima tupambane tupate matokeo chanya ili kujiweka sehemu nzuri zaidi ya sasa," amesema Maxime.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic