BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo, amesema kuwa sapoti anayopata kutoka Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Michezo, SportPesa inampa jeuri ya kuweza kupambana na bondia yoyote kwa sasa ambaye atahitaji pambano naye.
Mwakinyo, wikiendi iliyopita alifanikiwa kumpiga mpinzani wake raia wa Argentina, Sergio Gonzalez kwa KO katika raundi ya tano ya pambano hilo lililopigwa nchini Kenya lililokuwa lina raundi nane.
Mwakinyo amesema kuwa hivi sasa anafikiria kupigana mapambano ya kimataifa na siyo kitaifa kutokana na kutomuona bondia mwenye uwezo wa kupigana naye.
"Udhamini ninaoupata kutoka SportPesa hivi unanipa uhakika wa kufanya mazoezi mara mbili kwa siku huku nikiwa nina uhaika wa kupiga msosi wa maana.
“Binafsi sijaona bondia yeyote wa kupigana na mimi kwa bondia wa hapa bongo na hilo lipo wazi kutokana na kiwango changu nilichonacho hivi sasa.
“Nafahamu hivi sasa kila bondia anataka kupigana na mimi, lakini niwaambie kwangu sijamuona, kama yupo basi hamna shida ajiandae na uweke mkwanja wa kutosha utakaonishawishi kupigana," amesema Mwakinyo.
Mwakinyo ana mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya kubashiri ya SporPesa pia ni miongoni mwa mashujaa waliopewa zawadi na Serikali kutokana na kupeperusha Bendera ya Taifa.








0 COMMENTS:
Post a Comment