AZAM FC kesho watakuwa Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera kumenyana na Kagera Sugar chezo wa hatua ya robo fainali kombe la Shirikisho.
Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema wanatambua ushindani uliopo na namna ilivyo kazi kupata matokeo ila wana imani na jeshi kazi lililowafuata wapinzani wao.
"Hatuna cha kuhofia kwani tuna wachezaji wazuri na wapambanaji hasa linapokuja suala la kutafuta matoke, nia yetu ni kupata matoko chanya ili kusonga mbele kwenye hatua inayofuata.
"Hii ni vita ya ushindi kila mmoja anajua akishindwa anatolewa sasa kama ni hivyo basi hii ni sawa a fainali, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti nina imani kila kitu kitakwenda sawa," amesema Alando.
Azam wakimaliza mchezo wa FA watalazimika kwenda Mwanza kumalizana tena na Kagera Sugar mchezo wa ligi ikiwa ni mzunguko wa pili utakaochezwa Uwanja wa Nyamagana, Aprili 3.







0 COMMENTS:
Post a Comment