Kocha wa Lipuli, Seleman Matola amesema wachezaji
wake wanapaswa pongezi kwa namna wanavyopambana kupata matokeo chanya licha ya ugumu wanaopitia kwa sasa.
Lipuli jana ilipenya hatua ya robo fainali na kutinga nusu fainali baada ya kuwatungua mabao 2-0 Singida United mchezo uliochezwa Uwanja wa Samora.
Matola amesema kukosekana kwa mdhamini mkuu kwa sasa ndani ya ligi kunaziumiza timu nyingi hali inayofanya maisha kwa wachezaji na viongozi kuwa na changamoto nyingi ila bado wachezaji wake hawamuangushi.
"Umakini na utayari kwa wachezaji wangu unatubeba, bado kwa sasa mambo hayajawa sawa kwetu ila wananishangaza wanapata matokeo na wanapambana hivyo nawapongeza sana wachezaji wangu.
"Bado tuna safari ndefu kwa sasa maana ukishinda mchezo mmoja kuna mchezo mwingine mbele, sasa nimewaambia vijana wangu kwa sasa tujiandae na nusu fainali, nina imani tutapata matokeo kwa timu yoyote itakayopenya haitoki," amesema Matola.
Lipuli kwa sasa wanasoma ramani wakimsubiri mshindi wa mchezo kati ya Alliance na Yanga ndiye watacheza naye hatua ya nusu fainali, Uwanja wa Samora.







0 COMMENTS:
Post a Comment