LEO Droo ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) imefanyika ambapo timu nane zilizotinga hatua ya nane bora zimetambua zitacheza na nani hatua ya robo fainali.
Timu hizo ambazo zilitinga hatua hiyo ni pamoja na Yanga, Alliance FC, African Lyon, Azam FC, Lipuli, KMC na Kagera Sugar.
Michuano hii inatarajiwa kuanza mapema mwezi Machi itakuwa namna hii:-
Yanga wataifuata Alliance ya Mwanza Uwanja wa CCM Kirumba, Kagera Sugar wataikaribisha Azam Uwanja wa Kaitaba.
KMC wataikaribisha African Lyon Uwanja wa Uhuru.
Lipuli wataikaribisha Singida United Uwanja wa Samora.
Ingependeza Yanga kukutana na Azam!
ReplyDeleteIngependeza Yanga kukutana na Azam!
ReplyDeleteHii TFF iliitengenezea njia ya Yanga kushinda lakini hali imekuwa ngumu.Kwanza Yanga ilicheza mechi 11 nyumbani. Yanga haijacheza na Azam hata mechi moja wakingoja Azam apoteze matumaini ya ubingwa ndio mechi ipangiwe tarehe.
ReplyDeleteMechi ya Yanga na Azam ilipigwa kalenda bila sababu na kupanga Simba na Azam.
Yanga imepangiwa timu raundi ya pili karibu na timu zote isipokuwa Azam.
Unaelewa unachoongea au unataka tu uonekane. Hii ni kombe la FA siyo ligi kuu.
DeleteWewe unayelalamika, kwani Simba washacheza hata mechi moja na Mtibwa??
ReplyDelete