March 26, 2019

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, Jokate Mwegelo, amewataka Watanzania kuwa makini na matapeli wa mitandao kwani hana akaunti yoyote ya vikoba inayotoa mikopo kwa wananchi.

Jokate amesema kumekuwa na watu ambao wametengeneza akaunti  feki ambazo wanazitumia kufanya utapeli jambo ambalo hausiki nalo.

“Mimi sina akaunti yoyote ya vikoba na sijihusishi na jambo hilo, kwa vyovyote waliofungua akaunti hiyo kwa jina langu ni matapeli, wana nia ya kuwaibia wananchi hivyo wawe makini katika hilo.

Mkuu huyo wa wilaya kijana amesema amekuwa akipokea wageni mbalimbali wengine kutoka mikoani wakidai kwamba wametuma fedha kwenye akaunti hiyo feki ya vikoba.

“Tumepokea mtu kutoka Tabora anadai amefuatilia akaunti hiyo feki kwa sababu alituma fedha ili apate mkopo jambo ambalo halina ukweli, wananchi wasiwe wepesi kuamini hili halina ukweli," amesema Jokate.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic