March 26, 2019

BEKI wa timu ya Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' amesema kuwa kinachompa hofu ndani ya Dar ni hali ya hewa kuwa tofauti na Zanzibar.

Ninja ambaye kwenye ligi kuu amekuwa akitimiza majukumu yake ipasavyo ni miongoni mwa mabeki waliofungua akaunti ya mabao akiwa amefunga mawili mpaka sasa.

"Kitu kinachonipa hofu katika maisha ya Dar ni suala la joto, linanikwaza sana kwa sababu wakati mwingine unatoka mazoezini unaoga ila haipiti muda ushalowa inakubidi uonge tena.

"Jambo lingine ni suala la foleni tofauti na Zanzibar nilipokuwa naishi yaani naweza kwenda mazoezini hata kwa muda mchache ila hapa Dar safari ya dakika 10 itakuwa safari ya saa zima," amesema Ninja.

Yanga imepachika jumla ya mabao 45 baada ya kucheza michezo 28 imejikusanyia pointi 67 ni kinara wa ligi kwa sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic