March 30, 2019


KLAUS Kindoki leo amekuwa shujaa wa Yanga baada ya kuokoa penalti ya mwisho iliyopigwa na nahodha wa timu ya Alliance FC, Siraj Juma.

Dakika 90 za mchezo wa leo wa hatua ya robo fainali ulikamilika kwa Alliance kutoshana nguvu na Yanga kwa kufungana bao 1-1.

Yanga walitangulia kufunga bao dakika ya 38 lililofungwa na Heritier Makambo na kwa upande wa Alliance bao lilifungwa na Johson James.


Baada ya mwamuzi kuamua matuta, Yanga walianza kupiga kupitia beki kisiki Kelvin Yondani ambaye aligongesha kwenye mwamba, Paul Godfery alifunga penalti yake,Thaban Kamusoko alifunga kwa staili ya paneka, Mrisho Ngassa penalti yake iligonga mwamba na Haruna Moshi alifunga penalti kiufundi.

Kwa upande wa Alliance penalti ya kwanza ilifungwa na Joseph John, Martin Kigi aligongesha kwenye mwamba, Dickson Ambundo alikosa penalti yake, Jofrey Luseke alifunga penalti na Samir Vincent alifunga.

Baada ya kumaliza penalti 5 za awali kwa timu zote matokeo yalisoma 3-3 baada ya Yanga kukosa penalti mbili na Alliance pia kukosa penalti mbili. 

Hatua ya kupiga penalti mojamoja, Deus Kaseke alishinda penalti yake na kwa upande wa Alliance, nahodha Siraj Juma shuti lake liliokolewa na Kindoki. 

Kwa ushindi huo, Yanga wanatinga hatua ya nusu fainali na kuifuata Lipuli ya Matola kwenye hatua ya nusu fainali ya kwanza na ile ya pili itakuwa kati ya KMC na Azam FC.

3 COMMENTS:

  1. Ni Mganga kweli aloandika hii? Mbona leo hakuna makosa ya uandishi au ni furaha za timu yake kutinga nusu fainali....

    ReplyDelete
  2. Naona Leo Alikua Makini Naomba Niulize Kati Ya Saleh Ally Na Maganga Yupi Ni Mnazi Wa Yanga Hapo?

    ReplyDelete
  3. Huwezi jua ni nani anaandika habari za saleh jembe kwani huwa haandiki majina yao katika habari zao...unashitukia habari ya pumba yenye makosa ya kiuandishi impepostiwa tu! ila Leo wamejitahidi kwa kuwa Jangwani FC yao imeibuka kidedea kwa Alliance FC tena kwa matuta!Bahati yao itaendelea hivyo hadi mchezo unaofuata!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic