March 5, 2019


Kocha Mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Oscar Mirambo amesema pamoja na kupoteza mechi ya kwanza ya michuano ya Uesfa Assist kwa kufungwa kwa bao 1-0 dhidi ya Guinea, jana lakini bado wamejifunza.


Mirambo amesema mechi haikuwa nzuri katika kipindi cha kwanza kwa kuwa walipoteana na mambo hayakuwa mazuri lakini walibadilika na kufanya vema lakini wao wamejifunza kupitia makosa.

"Kuna makosa tulifanya, mfano bao lile, mabeki wa kati walichelewa kulifanyia kazi, hili ni kosa ambalo tusingependa kulirudia. Lakini kiungochetu kilikuwa na matatizo pia na hilo nalo tukalifanyia kazi kipindi cha pili.

"Kuna mengi ya kujifunza kwa kuwa kila unapocheza mechi kama hii inakusaidia kujiimarisha kwa lengo la kufanya vizuri katika mechi au michuano inayokuja," alisema Mirambo.


Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Emri Complex, ilitawaliwa na Guinea katika kipindi cha kwanza kabla ya Serengeti kuibuka katika kipindi na kuonyesha uhai katika kipindi cha pili.


Serengeti Boys  itashuka dimbani tena keshokutwa Jumatano kuwavaa Australia katika mechi ya pili ya Kundi Namba Moja itakayopigwa saa 9:30 Alasiri kwa muda wa hapa unaoendana na nyumbani Tanzania.

Mechi ya mwisho ya Serengeti Boys itakuwa dhidi ya wenyeji Uturuki.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic