UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo unakwea pipa kuanza safari ya kuwafuata wapinzani wao JS Saoura utakaochezwa Jumamosi, Machi 9 nchini Algeria.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanatarajia kuondoka na timu ya wachezaji 20 majira ya mchana huku mshambuliaji wao matata kwa waarabu Emmanuel Okwi akitarajiwa kuwa ndani ya msafara licha ya kusumbuiwa na majeruhi aliyoyapata katika mchezo wao dhidi ya Azam FC.
"Tunaondoka leo kuifuata JS Saoura , mchezo wa Ligi ya mabingwa ambao ni wa marudo, tunaamini utakuwa mchezo mgumu ila hamna namna ni lazima tukaiwakilishe nchi yetu.
"Tutaambatana na Okwi ambaye anasumbuliwa na majeruhi, kwa sasa ameanza kupata nafuu hivyo dua na maombi kwa mashabiki iambatane nasi tukienda kuiwakilisha nchi yetu kimataifa," amesema Manara.
Kila la kheyr
ReplyDeleteMunhu atajaalia kila la kheri na mtarejea nyuso juu zilizojaa furaha mkinyanyua karama ta Tanzania
ReplyDelete