March 9, 2019



FT: AS Vita 1- 0 Al Ahly 
Uwanja wa Stade des Martyrs. 

Dakika 90 zinakamilika zinaongezwa 3.
Dakika 89 Wang Bangu anaingia akichukua nafasi ya Tuisila Kisinda mfungaji wa bao la kwanza.

 Dakika ya 84 Tuisila Kisinda anaandika bao la kwanza baada ya kuachia shuti 

lililombabatiza beki na kumchanganya mlinda mlango wa Al Ahly na kufunga Goooooooooli la kwanza .

 Dakika ya 81 Jeremie Mumbere anaingia kuchukua nafasi ya J Makusu kwa AS Vita.

 Al Ahly wanaotea kwa mara kwanza kipindi cha pili dakika ya 78

 Dakika ya 75 Hussen El Shahat anaingia akichukua nafasi ya R. Sobhi.

 AS Vita wanapiga jumla ya kona 13 kwa sasa wakiwapa presha Al Ahly ambao wao wanapoza mashambulizi kwa sasa ikiwa ni dakika ya 74.

 Dakika ya 69 Walid Azaro anaingia anatoka Baruan Mohsen wa Al Ahly.

Ducapelo Moloco wa AS Vita anaingia dakika ya 66 akichukua nafasi ya R.Kasengu.

 Mlinda mlango wa AS Vita, Nelson Lukong langoni amekuwa ni kisiki ameokoa shuti kali dakika ya 63.

 Al Ahly wamepiga jumla ya kona nne kwa sasa ambazo hazijazaa matunda huku AS Vita wakiwa wamepiga kona saba.


Kipindi cha pili kimeanza kwa sasa kukiwa hakuna mabadiliko kwa vikosi vyote.

Al Ahly wanakosa nafasi mbili za wazi dakika ya 46 na mlinda mlango wa AS Vita anapewa huduma ya kwanza.

Mpira kwa sasa ni mapumziko.

 Dakika 45 zimekamilika zinaongezwa dakika 5. 

AS Vita wamepiga jumla ya ya kona sita ambazo hazijazaa matunda.


LIGI ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi mchezo unaoendelea kwa sasa katika kundi D ni kati ya AS Vita ya Congo na Al Ahly ya Misri, Uwanja wa Stade des Martyrs.

Dakika ya 20 mlinda mlango wa Al Ahly Mohamed Shenawy anapata majeraha baada ya kuanguka vibaya muda akiokoa hatari kwenye lango lake, anatolewa nje kwa machela nafasi yake inachukuliwa na Ali Mustafa dakika ya 23.

Al Ahly wanatumia mfumo wa 4-4-2 huku AS Vita wakitumia mfumo wa 4-2-3-1.

Mpaka sasa bado hakuna timu iliyoona lango la mpinzani kwa sasa.

AS Vita wanatafuta bao kwa kasi kwani wanafanya mashambulizi kwa kasi huku Al Ahly wakitengeneza mashambulizi kwa kushtukiza.

AS Vita dakika ya 44 wanaotea kwa mara ya kwanza.



Mchezo kati ya JS Saoura ya Algeria na Simba utapigwa saa nne Usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic