March 9, 2019


LIGI Kuu Tanzania Bara jana iliendelea kuwasha moto kwenye viwanja mbalimbali ambapo timu sita zilishuka Uwanjani kumenyana kutafuta pointi tatu ambapo timu tatu zilibeba point tatu mazima.

Lipuli FC ikiwa Uwanja wa Samora iliibuka kidedea mbele ya Mbao FC kwa ushindi wa bao 1-0, bao pekee la Lipuli lilifungwa na Jimmy Shoji dakika ya 32.

African Lyon ya Dar ilibanwa mbavu na Prisons ikiwa nyumbani Uwanja wa Uhuru, licha ya kuanza kufunga bao dakika ya 13 kupitia kwa Ramadhan Chombo, Prisons walipachika mabao mawili kipindi cha pili yote yakifungwa na Adam Adam dakika ya 51 na 69.

Mtibwa Sugar walitakata kwenye Uwanja wa Manungu mbele ya Stand United ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Stand.

Mbao ya Mtibwa Sugar yalipachikwa kimiani  kupitia kwa Riphat Khamis dakika ya 46 na Haruna Chanongo dakika ya 89.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic