MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, amesema mgeni rasmi katika kampeni ya Tokomeza Ziro, Machi 30 2019 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam atakuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani.
Jokate amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi siku kwenye kampeni hiyo inayolenga kuleta maendeleo ya elimu wilayani Kisarawe.
Amesema kampeni hiyo inakusudia kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana wilayani Kisarawe, mkoani Pwani.
“Tokomeza ziro ni kampeni ya kuhakikisha tunapanua elimu wilayani Kisarawe na tunaanza kwa kujenga shule ya wasichana, niwaombe wote wenye kutaka maendeleo ya elimu wajitokeze siku hiyo pale Mlimani City.
“Kuna changamoto nyingi kama vile mimba za utotoni kwa wasichana lakini tukijenga mabweni, tutakuwa tumepunguza tatizo kwa kiasi kikubwa.
Katika kampeni hiyo matarajio ya Jokate n kuona wengi wakijitokeza huku gharama kwa meza moja itauzwa kwa shilingi milioni moja.








0 COMMENTS:
Post a Comment